Tuesday, January 7, 2025

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UAPISHO WA RAIS WA GHANA MHE. JOHN MAHAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana kuhudhuria uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama leo tarehe 07 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama uliyofanyika katika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana wa tarehe 07 Januari 2025.
Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama akiapa kuwa Rais wa Taifa hilo katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana leo tarehe 07 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpongeza Rais wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra nchini Ghana leo tarehe 07 Januari 2025



No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake