RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha Nchi, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambuliwa wakielekea katika vituo vyao vya kazi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-4-2025 na (kulia kwa Rais) Mhe. Balozi Dkt. Habibu Kambanga Balozi wa Tanzania Nchi Rwanda, Mhe.Balozi CP.Suzane Kaganda Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mhe.Balozi Mobhare Matinyi Balozi wa Tanzania Nchini Sweden na Mhe. Balozi CP.Hamad Hamad Balozi wa Tanzania Nchini Msumbiji
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Mhe. Balozi Dkt.Habibu Kambanga, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-4-2025 na (kushoto ) Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe. Balozi Mabhore Matinyi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Nchi mbalimbali kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na Kuzitangaza fursa za Uwekezaji ziliopo.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Mabalozi wa Tanzania wa Nchi za Rwanda,Zimbabwe ,Sweden na Msumbiji Waliofika Ikulu kumuaga kabla ya kwenda katika Vituo vyao vya Kazi Baada ya kuteuliwa hivi karibuni.
Amewahimiza Mabalozi hao kufanya Juhudi Maalum za kuitangaza Sera ya Uchumi wa Buluu na Utalii katika Mataifa hayo Ili kuvutia Wawekezaji Zaidi kuwekeza Nchini.
Amesema Zanzibar bado inahitaji Wawekezaji wengi Hususan katika Sekta hizo Kuu za kipaumbele kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi ikiwemo Uvuvi,Utalii na Mafuta na Gesi.
Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Suala la Mahusiano ya Kimataifa hivi sasa limeelekezwa zaidi katika Uchumi hivyo wanapaswa kuzingatia zaidi Kuimarisha Uhusiano wa Kiuchumi.
Ameyataja Maeneo ambayo Yana fursa za kutosha kuwa ni Uwekezaji katika Sekta ya Bandari ikiwemo Bandari za Makontena ,Usafirishaji wa Mzigo, na Mafuta na Gesi.
Akizungumzia Sekta ya Biashara amewaagiza Mabalozi hao kuzitafutia Masoko Bidhaa za Tanzania ikiwemo Bidhaa za Viungo zinazozalishwa kwa Wingi hapa Zanzibar pamoja na Utalii wa huduma na Vivutio vya Utalii ili kuwavutia Watalii wa Mataifa hayo kutembelea Zanzibar.
Nao Mabalozi hao wameahidi kuyatumia Maelekezo ya Rais Dkt, Mwinyi kuwa ni nyenzo na dira ya kufanya Kazi zao kwa Ufanisi pamoja na kuyazingatia Maeneo Muhimu ya Kiuchumi kwa kuwashawishi Wawekezaji kuwekeza.
Mabalozi walioaga ni Balozi Dkt, Habibu Kambanga- Rwanda, Balozi CP Suzane Kaganda- Zimbabwe, Balozi Mobhare Matinyi - Sweden na Balozi CP Hamad Hamad - Msumbiji
No comments:
Post a Comment