Kardinali Kevin Joseph Farrell, ambaye ni Camerlengo alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francisko, kwa maneno haya: "kaka na dada wapendwa ni kwa huzuni kubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko. Saa 7.35 asubuhi ya leo, (Jumatatu 21 Aprili 2025), Askofu wa Roma, Francisko, alirejea nyumbani kwa Baba.
Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa Lake. Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa kupendelea maskini zaidi na waliotengwa zaidi. Kwa shukrani nyingi kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaiweka roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja na wa Utatu.”
Ilikuwa ni saa 9:47 asubuhi hii, ambapo Mwadhama Kardinali Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, alitangaza kwa masikitiko ya kifo cha Papa Francisko kwa waandishi wa habari
Na kufuatia tarifa ya kifo cha Papa Francisko, kama ilivyoelezwa katika Ordo Exsequiarum Romani Pontificis (nn. 21-40),yaani katika kanuni ya mazishi ya Papa wa Roma, “Jioni ya leo, Jumatatu tarehe 21 Aprili 2025 saa 2.00 usiku masaa ya Ulaya na (saa 3.00 kamili masaa ya Afrika Mashariki na Kati), Kadinali Farrell ataongoza ibada ya uthibitisho wa kifo na uwekaji wa mwili kwenye jeneza. Dekano wa Baraza la Makardinali, wanafamilia wa Papa, mkurugenzi na makamu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya na Usafi ya mji wa Vatican watashiriki katika ibada hiyo.
No comments:
Post a Comment