ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 17, 2025

WASIRA AMEKUTANA NA PROTASE KARDINALI RUGAMBWA


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akisalimiana na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa alipokutana naye katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, mjini Tabora April 16, 2025.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira Pipata maelezo kuhusu ofisi aliyoitumia Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa akifundisha Shule ya Sekondari St Marys (Mihayo) mjini Tanora baada ya kukutana na kuzungumza na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, mjini Tabora April 16, 2025. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Mkumba.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira akizungumza na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa alipokutana naye katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, mjini Tabora April 16, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Nzega

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kuanzia sasa hadi Oktoba mwaka huu kazi kubwa ya Chama ni kuhakikisha inakamata dola kwa nguvu ya wananchi.

Amesisitiza kwamba CCM haitegei Jeshi la Polisi kushinda uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Wasira aliyasema hayo jana alipokuwa akiungumza katika kikao cha ndani cha wanachama na viongozi wa CCM Wilaya ya Nzega na Igunga mkoani Tabora ambako anaendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CMM, kusikiliza kero za wananchi na kueleza maazimio ya mkutano mkuu maalum uliompitisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Akieleza hilo, Wasira alisema CCM ni Chama cha wakulima na wafanyakazi ambao hali zao zinajulikana huku akisema hao ndio wanaokihitaji zaidi Chama kuwasemea changamoto zao.

Aliwaomba wana CCM kuwasikiliza wananchi na kwamba kuanzia sasa hadi Oktota kazi yao kubwa ni kuhakikisha Chama kinakamata dola.

“Tunaikamata dola sio kwa nguvu ya Jeshi la Polisi bali kwa nguvu ya wananchi, tumewasikia wengine wanasema unajua hawa hawashindi bila jeshi…wapi! Mbona wao waliwahi kushinda hata Tundu Lissu alishinda pale Jimbo la Singida Mashariki kwani alikuwa na jeshi? Ameshinda mara mbili jeshi lilikuwa limeenda wapi? Uongo tu!

“Nimeshawaambia kulalamika ni kazi rahisi na ingelikuwa watu wote wanataka ajira ya kulalamika kila mtu angeipata maana hakuna anaeshindwa. Wao wamejikita katika kulalamika lakini hawana maelezo, tumesikia mambo wanayosema huko.

“Oooh wanataka 'reform' mbona 'reform' tumefanya juzi tulikuwa nao Aprili 2, mwaka huu, mimi nilikuwa kwenye kikao cha Kituo cha Demokrasia Tanzani (TCD) kuna vyama vitano vyenye wabunge na madiwani tumekutana tena uenyekiti wa kituo kile tunapeana zamu.

“Katika kikao ambacho Mwenyekiti alikuwa Tundu Lissu ndio mara ya kwanza, nikajiuliza sijui kitaisha salama? Lakini kikaisha salama tukapitia matatizo ya vyama vyote, tukakubaliana wakuu wa vyama hivi wakutane halafu wapendekeze kitu gani tupeleke kwa mamlaka ya uchaguzi kuleta uboreshaji ambao unatakiwa uchaguzi uwe huru na wa haki," alisema.

Alisema baada ya kikoo hicho walikubaliana kukutana tena Aprili 12 kwa utiqji saini kanuni za maadili ya uchaguzi mkuu, lakini kabla ya kufika siku hiyo viongozi wa CHADEMA walienda walikoenda 'wakalikoroga' na sasa kuna mambo ambayo hawezi kuyazungumzia kwa kuwa yako mahakamani.

“Tumeongeza mambo ambayo ni ya kiutawala ambayo tunasema haya yakiondoka tutakuwa na nafuu, nani hataki nafuu? Huu Mkoa wa Tabora ni mkoa wa 11 tangu nilipochaguliwa kuwa makamu mwenyekiti. Nimekutana na watu wengi wakiwemo wakulima na watu wa makundi mengine.

“Hali ya Dk. Samia na CCM ni nzuri wala hatuhitaji polisi kutusaidia kushinda uchaguzi, watu wanatukubali, wana CCM hawadanganyiki. Tumewapa maji akinamama, tumewatua ndoo kichwani, wanatupigia kura…tumejenga hospitali, vituo vya afya, tumeweka magari ya kubeba wagonja, tumenunua vifaa tiba vya kısasa.

“Halafu mtu aliyepata huduma nzuri namna hii aache kutupigia kura CCM aende akapigie kura chama cha watu wanaogombana labda atakuwa amepata kichaa! Maana hata kupiga si unapigia matumaini yako, sasa matumaini yako katika chama gani? Kwa hiyo mimi ninaamini CCM tunayo nguvu ya kushinda tena katika uchaguzi huru na wa haki.

“Kwa hiyo wale ambao wako tayari kuja kufanya uchaguzi na sisi tunawakaribisha, hakuna tatizo tutakuwa wawazi na wakweli, kampeni za wazi wazi, tutatangazwa mahali panapostahili kutangazwa na wao watatangazwa, watapiga kura tutahesabu na wao mawakala wao watakuwepo.

“Hivyo CCM hatuna Mashaka na uchaguzi Mkuu mwaka huu na hao wanaosema uongo kwamba CCM hatushindi bila Jeshi la polisi ni kuwapuuza.Kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tunaomani Watanzania watatuchagua na nguvu yetu ya ushindi na kushika dola inatokana na wananchi.”

No comments: