Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni mhimili muhimu katika mapambano dhidi ya uhalifu wa dawa za kulevya nchini Tanzania. Katika hatua za awali za uchunguzi wa mashauri ya dawa za kulevya, Ofisi hii hushirikiana kwa karibu na vyombo vya upelelezi pamoja na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuhakikisha ushahidi unakusanywa ipasavyo kabla ya kufikishwa mahakamani. Lengo ni kuhakikisha haki inatendeka kwa misingi ya ushahidi wa kisayansi na kisheria.
Katika kuhakikisha ufanisi wa mashauri haya, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mashauri yote ya dawa za kulevya yanakamilika kwa hukumu ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita.
Tangu Julai 2024 hadi Juni 2025, jumla ya mashauri 2,785 ya dawa za kulevya yalipelekwa mahakamani ambapo Jamhuri ilishinda mashauri 2,021, sawa na asilimia 63%. Katika kipindi hicho hicho, mafanikio ya jumla ya mashitaka yote ya jinai yaliyosimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ma kusinda yalifikia asilimia 72%.
Hii ni dalili ya utendaji mahiri na juhudi zinazostahili pongezi katika kulinda usalama wa jamii dhidi ya janga la dawa za kulevya.
Kauli mbiu: "Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya"
#DCEA
#OktobaTunatiki
No comments:
Post a Comment