Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila), Dkt. Delilah Kimambo, leo Juni 10, 2026, amefungua rasmi Kikao cha 31 cha Baraza la Wafanyakazi kinachowakutanisha wawakilishi wa watumishi kutoka idara na vitengo mbalimbali vya hospitali kujadili masuala ya maendeleo ya taasisi na ustawi wa watumishi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Dkt. Kimambo amewataka wajumbe kutumia jukwaa hilo kutoa mawazo na mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha utendaji wa hospitali na kuboresha huduma za afya kwa wananchi na kusisitiza kuwa mafanikio ya Muhimbili yanategemea mshikamano, uwajibikaji na ushirikiano wa watumishi katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujituma.
Baraza la Wafanyakazi Muhimbili hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili na kutathmini utekelezaji wa shughuli za hospitali, kupitia mipango na bajeti ya taasisi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya menejimenti na watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.









No comments:
Post a Comment