ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 1, 2026

ETHIOPIA IMEFANIKIWA KUINGIZA MBUNGE WA PILI MWENYE ASILI YA ETHIOPIA KATIKA BUNGE LA MAREKANI (U.S. CONGRESS).

MOHAMED MATOPE, Washington, DC

Jana, Melat Kiros, mwanamke mwenye umri wa miaka 29, aliandika historia baada ya kumshinda mbunge aliyekuwa madarakani kwa takribani miaka 30 katika uchaguzi wa mchujo (Democratic Primary) uliofanyika Denver, Colorado. Ushindi huo umeonekana kuwa moja ya matokeo makubwa zaidi ya kisiasa mwaka 2026.

Kwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura katika jimbo hilo huunga mkono Chama cha Democratic, Kiros anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu mwezi Novemba na kuwa Mbunge wa pili aliyezaliwa Ethiopia kuhudumu katika Bunge la Marekani.

Melat Kiros, a corporate attorney, alizaliwa Addis Ababa, Ethiopia, na alihamia Marekani akiwa mtoto mchanga baada ya familia yake kupata nafasi kupitia mpango wa Diversity Visa Lottery. Alikulia katika jimbo la Colorado, ambako alifanya vizuri katika masomo na baadaye akapata shahada ya Political Science na Economics. Baadaye alihitimu shahada ya sheria (Juris Doctor,J.D.), na kwa sasa ni mwanafunzi wa Ph.D. katika Public Policy katika University of Colorado Denver.

Mafanikio yake pia yanaonyesha umuhimu wa nchi za Afrika kuwatambua Diaspora, kuwapa haki za kiraia na nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa lao. Diaspora ni rasilimali muhimu yenye mtandao mpana wa ushawishi, utaalamu na fursa zinazoweza kutumika kuitangaza na kuitetea nchi kimataifa.

Waswahili husema, Usipokuwa mezani, utaishia kwenye menyu. Kwa sasa, Ethiopia ina watu wawili waliozaliwa nchini humo na kwa kuwa nchi yao inaruhusu uwepo wa uraia pacha, ni raia wa nchi hio, walioshikilia na wanatarajiwa kushikilia viti katika Bunge la Marekani. Hiyo ina maana ya kwamba, kuna sauti za Ethiopians kwenye meza kubwa kupita zote duniani, mahali ambapo maamuzi muhimu kuhusu sera za Marekani na uhusiano wake na mataifa mengine hufanyika. Ingawa wabunge hao wanawakilisha wananchi wa majimbo yao na maslahi ya Marekani, uelewa wao wa historia, utamaduni na changamoto za Ethiopia unaweza kuchangia kujenga daraja la maelewano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mafanikio ya Melat Kiros ni fahari kwa Ethiopians na Africans na diaspora wote wanaoamini kuwa ndoto zinaweza kutimia kupitia elimu, kazi ngumu na huduma kwa jamii. Pia ni ukumbusho kwamba kuwekeza katika watu wako, hata wanapoishi nje ya nchi, kunaweza kuzaa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika jukwaa la kimataifa.


 

No comments: