Hafla ya JKCI–HTAF Prestige Gala Dinner 2026 inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kugharamia matibabu ya moyo kwa watoto na kujenga Nyumba ya Matumaini.
TANZANIA inakabiliwa na changamoto ya watoto wanaozaliwa na matatizo ya moyo, hali inayohitaji ushirikiano wa Serikali, sekta binafsi, taasisi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha watoto wenye uhitaji wanapata huduma za matibabu kwa wakati.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF), inalenga kukusanya shilingi bilioni 25 kupitia hafla ya JKCI–HTAF Prestige Gala Dinner 2026, itakayofanyika tarehe 4 Desemba 2026 katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza, chini ya kaulimbiu “Okoa Moyo wa Mtoto, Okoa Taifa.”
Fedha hizo zinalenga kusaidia matibabu ya watoto 1,000 wenye matatizo ya moyo katika kipindi cha miaka 4 hadi 5, pamoja na kugharamia vipengele vingine vya mpango huo, ikiwemo ujenzi wa Nyumba ya Matumaini, itakayosaidia watoto wanaopatiwa matibabu na familia zao.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makadirio yaliyotolewa yanaonesha kuwa watoto 16,000 hadi 24,000 wanaweza kuzaliwa na matatizo ya moyo nchini kila mwaka. Kati yao, takribani watoto 4,000 wanakadiriwa kuwa na magonjwa makali ya moyo yanayohitaji upasuaji ndani ya mwaka mmoja
Changamoto inayowakabili baadhi ya watoto hao si ukosefu wa wataalamu , bali pia uwezo wa familia kugharamia sehemu ya matibabu inayobaki baada ya mchango wa Serikali.
Serikali ya inagharamia asilimia 70 ya gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo, huku mzazi au mlezi akiwajibika kugharamia asilimia 30 inayobaki. Hata hivyo, kutokana na hali ngumu za kiuchumi, familia nyingi hushindwa kumudu sehemu hiyo ya gharama, jambo linaloweza kuchelewesha watoto kupata huduma wanazohitaji.
Akizungumzia umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, amesema Tanzania ina wataalamu na uwezo wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake