Tatu Hassan (23), mkazi wa Sangoma, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, kwa miaka minne aliishi na uvimbe mkubwa chini ya taya uliomsababishia maumivu makali na msongo mkubwa wa mawazo, na kufikia hatua ya kukata tamaa na kutamani kufa.
Kupitia utaalamu wa Madaktari Bingwa na Bobezi pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) iliweza kumtibu na kumrejeshea matumaini ya kuendelea na maisha.
Ambatana naye katika simulizi hii.

No comments:
Post a Comment