Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga amemuomba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kusaidia kutatua mgogoro unaokumba serikali ya muungano nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ambaye ni mshirika wa karibu wa Bw.Odinga amesema mgawanyiko umezuka baada ya rais kubatilisha uamuzi wa Waziri Mkuu wa kuwasimamisha kazi mawaziri wa elimu na kilimo kufuatia kashfa za ufisadi.
Annan alisaidia kuafikiwa kwa muafaka wa kuundwa serikali ya muungano Kenya. Hatua hiyo ilisaidia kumaliza machafuko ya baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha.
Huku haya yakiarifiwa mawaziri hao William Ruto na Profesa Sam Ongeri waliendelea na kazi zao kama kawaida.Wawili hao wametuhumiwa kwa ubadhirifu wa mamilioni ya dola fedha za umma.

No comments:
Post a Comment