Adedisha wife,Kisa kupika ugali mwingi!
Leticia Protus (22) mkazi wa kitongoji cha Omurungu, Kata ya Minziro, Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, ameuawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na husband wake, kwa sababu ya kupika ugali mwingi.Mume huyo mwenye ukatili usiopimika na kipimo cha aina yoyote alifanya unyama huo Machi 12, majira ya saa 4 asubuhi...eti kosa ni kuchukizwa na na tabia ya mke wake kupika chakula kingi.
Hata hivyo, Polisi walisema mtuhumiwa huyu alitoweka kusikojulikana mara baada ya kufanya unyama huo, hali iliyosaidia marehemu kupata mwanya wa kukimbilia kwa kaka yake, John Protus, huku akilia na kusema mumewe anamuua.
Kaka wa marehemu kwa kushirikiana na majirani waliamua kumkimbiza hospitali kwa matibabu lakini kabla hawajafika alifariki dunia.
No comments:
Post a Comment