ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 18, 2010

Mahakama ya ICTR yatupilia mbali rufaa ya Bikindi

Mwanamuziki Simon BikindiMahakama ya Kimataifa inayochunguza mauaji ya Kimbari nchini Rwanda ICTR, imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na mwimbaji maarufu wa Rwanda Simon Bikindi, kupinga hukumu aliyopewa ya miaka 15 gerezani.
Bikindi alipatikana na hatia ya kuchochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Jopo la majaji wa mahakama ya Rufaa kwenye mahakama hiyo, iliyoko mjini Arusha Tanzania, wamepuuzilia mbali rufaa ya Bikindi.
Mahakama hiyo, vile vile imekataa ombi la waendeshamashtaka la kutaka hukumu dhidi ya mwimbaji huyo kuongezwa zaidi. Mwaka wa 2008, mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, ilimpata na hatia Bikindi kwa kutoa hotuba iliyowachochea Wahutu kuwaua Watutsi.

No comments: