ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 19, 2010

Capello amwalika Beckham Afrika Kusini


David Beckam of AC Milan on the bench looks on before the Serie A match between AS Roma and AC Milan at Stadio Olimpico on March 6, 2010 in Rome, Italy.England Manager Fabio Capello arrives at the Laureus World Sports Awards 2010 at Emirates Palace Hotel on March 10, 2010 in Abu Dhabi, United Arab Emirates.Kocha wa England Fabio Capello amemualika David Beckham kujiunga na kikosi cha England cha Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini licha ya kiungo huyo kuwa ameumia.
Capello ameiambia televisheni ya Gol "Tumemwambia Beckham aambatane nasi kuelekea Afrika Kusini."
Ameendelea kufahamisha"Inategemea na yeye mwenyewe na namna jeraha lake lilivyo. "Ni wazi hatoweza kucheza kwa sababu itambidi asubiri kwa miezi sita."
Beckham alifanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu nchini Finland, lakini nahodha huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 34, hatokuwa katika nafasi ya kucheza Afrika Kusini.
Capello pia amesema bado mlizi wa kushoto wa Mnchester City Wayne Bridge anayo nafasi kufikiria upya uamuzi wake wa kuichezea England.

No comments: