
Serikali ya Ethiopia imekiri kuchukua hatua za kuzuia kituo cha radio cha Marekani, VOA, Kupeperusha matangazo yake nchini humo.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi, ameishutumu idhaa ya lugha ya Amharic ya VOA, kwa kusambaza habari za uchochezi ambazo zinaweza kutikisa uthabiti wa taifa hilo.
Zenawi amefananisha matangazo ya kituo hicho na yale yaliyopeperushwa nchini Rwanda, miaka ya tisini kuchochea mauaji ya halaiki.
Wakati huo huo Zenawi, amekanusha habari zilizotangazwa na BBC kuwa aliagiza, kutumiwa kwa pesa za vyakula vya misaada, kununua silaha ili kupambana na serikali ya Mengistu Haile Mariam miaka ya themanini.
No comments:
Post a Comment