ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 19, 2010

Taliban 'wakaribisha' mazungumzo ya amani


Mjumbe wa zamani wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Kai Eide amekashifu Pakistan kwa kuwashika viongozi wa Taliban.
Bw Eide amekiri kuwa, kwa mwaka mzima amekuwa akifanya mikutano na viongozi wa ngazi za juu wa kundi la Taliban, mjini Dubai na sehemu zingine.
Mjumbe huyo amesema kuwa mikutano hiyo ilikuwa imeridhiwa na kiongozi wa Taliban Mullah Omar.
Bw Eide ambaye ndio amestaafu kutoka wadhifa huo, amesema hatua ya Pakistan imehujumu juhudi za kuleta amani nchini Afghanistan.
Katika mahojiano na BBC, alikiri kuwa mikutano hiyo iliongezeka miezi michache iliopita lakini hawajakutana tena baada ya Pakistan kuwashika viongozi wao.
Watu kadhaa wamehoji hatua hiyo ya Pakistan ya kuwashika viongozi hao wakati huu, il hali kwa muda mrefu viongozi hao wamekuwa wakiishi salama nchini humo.
Madai ya Bw Eide yanaonyesha kuwa Pakistan haitaki mtu mwengine yoyote aongoze mazungumzo hayo na kuwa huenda vigogo wa kundi la Taliban wanapendelea mazungumzo ya amani.

No comments: