
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Larvov, amesema mashambulio ya kujitoa mhanga mjini Moscow hapo jana yameonyesha haja ya kuwepo kwa ushirikiano zaidi wa kimataifa ili kuzuia mashambulio kama hayo.
Akiongea katika mkutano wa mataifa nane tajiri duniani G-8, Bwana Lavrov ametoa wito kwa viongozi wa kimataifa kujitolea kupambana na mitandao ya magaidi duniani.
Naye Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, amesema mashambulizi hayo ya Moscow, yameonyesha kuwa dunia inakabiliwa na adui mmoja.
Takribani watu thelathini na wanane waliuawa, wakati wanawake wawili walipolipua mabomu waliokuwa nayo karibu na treni mjini moscow, jana asubuhi.
Maafisa wa serikali wamelaumu makundi ya Waislamu Kaskazini mwa nchi hiyo kwa kutekeleza mashambulio hayo. Waasi wa maeneo hayo wamekuwa wakipamabana na vikosi vya usalama wakitaka kujitenga na Urusi. Serikali ya nchi hiyo imeapa kuwasaka na kuwaangamiza waliotekeleza mashambulio hayo
No comments:
Post a Comment