
Mahakama moja ya kiislamu nchini Nigeria imeipiga marufuku kundi moja la kutetea haki za binadamu kwa kuwa na mjadala kwenye wavuti juu ya kutoa adhabu ya kukatwa viungo.
Hatua hii inafuatia agizo la muda lililotolewa wiki iliyopita na mahakama kaskazini mwa Nigeria kuzuia mtandao wa Facebook na Twitter kutumiwa kujadili suala hilo.
Awali marufuku hiyo ilipendekezwa na kundi moja linalounga mkono Sharia lililosema wavuti zitatumika kukejeli sheria za kiislamu.
Sheria za kiislamu zinafuatwa pamoja na sheria zisiokuwa na uhusiano wa kidini katika majimbo 12 kati ya 36 nchini humo.
No comments:
Post a Comment