Viongozi wa makundi ya upinzani nchini Sudan wanakutana kujadili ikiwa watashiriki katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 16 April.
Tayari wajumbe wa chama cha SPLM wanakutana kujadili msimamo wao kuhusu uchaguzi huo.
Makundi ya upinzani ya kaskazini mwa nchi hiyo tayari yametoa wito uchaguzi huo uhairishwe kutokana na hofu kwamba hautakuwa wa hura na haki.
Mazungumzo ya leo huenda yakasababisha kundi la waasi wa zamani wa kusini mwa sudan, SPLM, kuungana na makundi hayo kususia uchaguzi.
Uchaguzi wa April utakuwa ni uchaguzi wa kwanza kuwahi kufanyika nchini sudan kwa kipindi cha miaka 24 iliyopita.
No comments:
Post a Comment