
Mabomu mawili yaliyolipuliwa na mlipuaji wa kujitolea mhanga katika eneo la Urusi la Dagestan - Kaskazini mwa Caucasus, yamewaua watu 12, miongoni mwao akiwa kiongozi wa jeshi la polisi na maafisa wake kadhaa.
Mmoja wa walipuaji hao alitegua bomu lake aliposimamishwa na maafisa wa polisi na kuamrishwa kuliegeza gari lake pembeni.
Mwingine aliyekuwa amevalia sare rasmi za polisi, alijilipua alipokuwa akikaribia mahali ulipotokea mlipuko wa kwanza.
Waziri Mkuu wa Urusi, Vladmir Putin, amesema kuwa milipuko hiyo huenda ina uhusiano na milipuko mingine miwili iliyowaua watu 39 mjini Moscow Jumatatu.
No comments:
Post a Comment