ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 31, 2010

                   MSIBA




Familia ya Mzee Augostino Lissu Mughwai wa Mahambe, Singida inasikitika kutangaza kifo cha mama  yao mpendwa Martha Alu Alute kilichotokea tarehe 30 Machi, 2010 huko Dar es Salaam, Tanzania. Maandalizi yanafanywa kusafirisha mwili wa marehemu Mahambe, Singida kwa mazishi. 

Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Ighuka, Singida. Ameacha mume na watoto nane: Alute Mughwai wa Arusha, Tundu Lissu, Mjengi Lissu na Christina Lissu wa Dar es Salaam, Rose Masesa wa Songea, Peter Muro Mughwai wa Kondoa, Mateo Mughwai wa Singida na Vincent Lissu Mughwai wa Connecticut, Marekani. 

Vile vile marehemu ameacha wajukuu 20, na vitukuu 6.

Kwa marafiki wa wafiwa wanaokaa nje ya Tanzania (Marekani, Uingereza n.k) unaweza kutuma rambirambi zako kwenye accnt # 1259458568, routing #221172610.

Au kwenye anwani ifuatayo: Vincent Mughwai 370 Huntington Road 2F Bridgeport CT 06608

No comments: