Simba (Lunyasi)
Afisa ubalozi amekubali mualiko kuwa mgeni rasmi kwenye kindumbwe dumbwe cha Simba na Yanga,mechi inayozungumziwa mjini Washinngton na vitongoji vyake,
Yanga Imara
Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 kwenye wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,kambi zote zipo shwari na zinaendelea vizuri na mazoezi.Simba inaonekana imejiimarisha zaidi baada ya wachezaji wengi wa mikoani akiwemo Francis Makalaa aliyewahi kuichezea Simba miaka ya Nyuma kuthibitisha kuwepo kwenye mpambano huo,Kuhusu Nteze John bado viongozi wa Simba wanaendelea kumtafuta kwa udi na uvumba,Nteze anaishi Washington State alisahawahi kua mchezaji wa kutumainiwa Simba na Timu ya Taifa.kabla hajajiunga na Simba,alikua mchezaji wa Pamba ya Mwanza.
Stars United
Kambi ya Yanga imekua kimya Kocha Yasini Randi amesema Simba wacha waongee,msema ukweli dakika 90,sisi bwana tupo tunaendelea vizuri na kambi yetu,sisi tunaingia uwanjani kama YANGA IMARA KUFUNGWA DAIMA MWIKO
Jumamosi April 3 kutakua na mechi nyingine ya Stars na Maryland untd,itakayochezewa
18031 central park circle,
Boyds,Md,20841,uwanja # 20
mechi hii ni moja ya mechi za kujinoa ya Stars kwa safari ya kuelekea Sweden july mwaka huu,mechi nyingine ya Stars ni April 24 mjini Boston itapambana na Zambia
Maryland United
No comments:
Post a Comment