ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 30, 2010


Maximo na kijasho chembamba


Mara baada ya kuicharaza timu ya Somalia mabao 6-0, Kocha Mkuu wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Marcio Maximo azidi kuwahofua wapinzani wake Rwanda, Amavubi watakayokutana nao uso kwa uso hapo Mei Mosi hapa kwa Lukuvi.



Maximo alisema kwamba ile safari ya kuelekea katika fainali zijazo cha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN, inatarajiwa kuanza pindi watakapokutana na Rwanda na kwamba mechi hiyo ya juzi ilikuwa ni kama mazoezi.

Alisema kwa sasa timu yake ina kazi kubwa ya kuhakikisha wanaifunga Rwanda, ili kuweza kupata tiketi hiyo ya kushiriki katika fainali hizo za pili zitakazofanyika nchini Sudan mwakani.

"Rwanda wana timu nzuri na mara nyingi huwa na ushindani tunapokutana. Fainali yetu itakuwa ni Kigali tutakaporudiana na si katika mechi ya kwanza itakayofanyika hapa nchini. Nadhani kila shabiki anaifahamu Rwanda inapokuwa nyumbani kwao," alisema Maximo.

Timu ya Stars itazidisha mazoezi katika kujiandaa na mechi hizo mbili, na wanaamini kwamba kila mchezaji anafahamu ugumu unaokuwepo wanapokutana na Rwanda.

Alisema kwamba wakati wote walipokuwa wanajiandaa na Somalia, mawazo ya wote yalikuwa yako mbele zaidi kwa kuitazama Rwanda, kwa sababu walifahamu kwamba ndipo mahala ambapo mashindano hayo yanaanza rasmi kwao.

Kwani mechi ya Stars na Rwanda itakuwa ngumu kutokana na timu hizi kufahamiana zaidi, huku kila timu ikipata ushirikiano mkubwa kutoka katika serikali yake.

Naye Nahodha wa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro', alisema kwamba wao wana uzoefu na mechi za kimataifa tofauti na wachezaji wa Rwanda ambao wengi wametoka katika timu ya vijana ya U-20 ya nchi hiyo.

Cannavaro alisema kwamba mwaka huu wako makini zaidi na hasa ukizingatia kwamba fainali hizo husaidia kuwatangaza wachezaji.

Stars na Rwanda iliyokuwa chini ya mzawa, Eric Nshimiyimana, mara ya mwisho zilikutana katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika Desemba mwaka jana jijini Nairobi Kenya, ambapo Kilimanjaro Stars ilikubali kipigo cha magoli 2-0.

Na timu mbili za ukanda huu ambapo ni mshindi baina ya Taifa Stars na Amavubi, na wa mechi nyingine baina ya The Cranes na Harambee Stars ya Kenya, ndio zitawakilisha ukanda wao katika fainali zijazo za CHAN.



No comments: