Uwanja wa ndege wafungwa,Kisa PANYABUKU!
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Queen Mlozi ameiomba serikali ya JK kuitengea wilaya hiyo fedha angalau kiduchu ktk bajeti ya mwaka huu ili waweze kukarabati uwanja wao wa ndege ambao umeathiriwa ile mbaya na panyabuku kiasi cha kuamuliwa ufungwe.
Uwanja wa Ndege wa Nkilizya ulifungwa mwaka 2007 baada ya ndege ndogo tatu kuharibika wakati zikitua uwanjani hapo kutokana na njia ya uwanja huo kujaa mashimo ambayo ni makazi ya kudumu ya panyabuku hayo.
Ombi hilo limetolewa na mkuu huyo wa wilaya wakati alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawlance Masha alipotembelea na kukagua eneo la uwanja huo kujionea hali ya usafiri wilayani Ukerewe
No comments:
Post a Comment