![]() |
| Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, Fred Mpendazoe, (Katikati) akiwa katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana wakati akitangaza kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ), Picha na Mwandishi Wetu Katika tukio nadra, chama tawala nchini Tanzania, CCM, kimepoteza mbunge mmoja ambaye amehamia chama kipya cha upinzani. Mbunge huyo, Fred Mpendezoe, ametangaza kujiunga na Chama Cha Jamii yaani CCJ kilichopewa usajili wa muda hivi karibuni. Bw Mpendazoe amekuwa miongoni mwa wabunge wenye kukosoa wazi hitilafu ndani ya CCM. Kumekuwa na uvumi mwingi kwamba chama hicho kitazoa vinara wa CCM. Hata hivyo, chama chake alichokihama, kimesema hakiona lolote la ajabu kutokana na hatua ya Bw Mpendazoe. Makamu wa mwenyekiti wa CCM, Bw Pius Msekwa, alipohojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alisema kuondoka kwa Bw Mpendazoe ni kama mto Rufiji kupoteza ndoo moja tu ya maji, na kamwe hilo ni jambo ambalo halitakiathiri chama kwa njia yoyote. Vile vile alisema mbunge huyo ana uhuru wa kukihama chama, kulingana na katiba ya CCM. |
ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, March 30, 2010
Mbunge wa CCM ahamia upinzani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment