ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 18, 2010

Mfalme Albert wa Ubelgiji kuzuru DRC


 AlbertII.JPG Ikulu ya kifalme mjini Brussels Ubelgiji, imesema Mfalme Albert wa Pili atahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilipojinyakulia uhuru wake kutoka Ubelgiji.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka ikulu hiyo, Mfalme Albert na mkewe wamekubali mualiko kutoka kwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, kuzuru nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu.
Kwa zaidi ya miongo miwili Congo, ilitawaliwa kama himaya ya kibinafsi ya mfalme wa Ubelgiji, Leopold wa pili, ambaye alijilimbikizia utajiri mkubwa kutokana na mauzo ya zao raba.
Watafiti wa historia wanasema mamilioni ya raia wa Congo waliuawa wakati wa utawala wa mfalme Leopold wa pili.

No comments: