ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 18, 2010

Polisi Afrika Kusini walaumiwa kutisha watoto


Polisi wa Afrika Kusini wamewafyatulia risasi za mpira watoto wa shule waliokuwa wakiandamana kumlaani mwanamuziki mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kusababisha vifo.
Molemo Maarohanye, maarufu kwa jina la Jub Jub, anashutumiwa kwa kuua wanafunzi wanne wakati wa mashindano ya kukimbiza magari.
Makundi ya watoto walikusanyika nje ya mahakama ya Soweto na kurusha mawe, wakiwa wamebeba mabango na kutoa vitisho vya kumuua mwanamuziki huyo.
Idadi kubwa ya maafisa wa polisi walifika eneo la tukio, kabla ya kuwakamata baadhi ya wanafunzi na kuwatawanya wengine.
Shirika la habari la Afrika Kusni SAPA limesema kuwa viongozi wa wanafunzi walilazimika kuhutubia umati huo kutuliza jazba ya vijana hao.
Kwa wakati fulani, baadhi ya watoto waliimba kuwa wangemuua mwanamuziki huyo alipoonekana akiondoka mahakamani hapo.

No comments: