ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 18, 2010

Urusi, Marekani kujadili upunguzaji wa silaha

Hilary Clinton waziri wa kigeni wa MarekaniWaziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Hilary Clinton anatarajiwa kuwasili mjini Moscow kwa ziara ya siku mbili, ambapo atashiriki mazumgumzo ya Mashariki ya Kati, pamoja na kujadiliana na maafisa wa urusi juu ya mkataba wa kupunguza silaha za nuclear.
Maafisa wa Marekani wanaosafiri pamoja na waziri wa mambo ya nje, wanataraji kuwa mikutano kati ya Bi Hilary Clinton na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yatasaidia kukamilisha mkataba wa kupunguza silaha za nuclear.
Walisema kuwa mazungumzo yanayohusu Urusi, mikataba huwa inahitaji hali kama hiyo ya kuendeshwa na maafisa wa ngazi za juu.
Washington na Moscow walitaka kukamilisha mkataba huo ifikapo mwisho wa mwaka huu, baada ya mkataba wa siku za nyuma wa START muda wake kumalizika.
Afisa mmoja alisema kuna maendeleo makubwa yaliyopatikana, lakini akaongeza kuwa kila wanapopodhani wamekamilisha mambo, masuala mapya hujitokeza.
Rais Barack Obama angependa muafaka huo ukamilishwe kabla ya mkutano wa viongozi wa dunia juu ya kudhibiti usambazaji wa silaha za nuclear, ambao utafanyika mjini Washington mwezi ujao.

No comments: