Kiongozi wa kundi la waasi wa Chechnya, Doku Umarov, amesema kundi lake lilihusika la mashambulio mawili ya mabomu kwenye treni za chini ya ardhi mjini Moscow, ambako watu 39 waliuawa.
Katika ujumbe wa video uliowekwa kwenye tovuti ya waasi wa Chechnya, alisema yeye binafsi aliagiza kufanyika mashambulio hayo.
Alisema mashambulio yalifanyika kulipiza kisasi dhidi ya majeshi ya Urusi mwezi Februari, yaliyoua "Wachechen wasio na hatia" na ameionya Urusi ijiandae kwa mashambulio zaidi.
Wachunguzi wa Urusi wamesema wanaamini walipua mabomu wawili wa kujitolea muhanga ambao ni wanawake walihusika na wanahusiana na wanamgambo wa eneo la North Caucasus.
Waziri Mkuu Vladimir Putin ametoa wito kwa majeshi ya usalama "kuwaangamiza" wale waliohusika na mashambulio.
No comments:
Post a Comment