ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 31, 2010

Aliyechoma makaburi Uganda ajisalimisha


Mtu mmoja amejisalimisha kwa polisi nchini Uganda na kukiri kuchoma moto makaburi ya wafalme wa kimila wa Baganda mapema mwezi huu.
Mtu huyo anadai aliambiwa achome makaburi kwa njia ya maono na kusema makaburi yalikuwa ya kishetani.
Falme hiyo ya Baganda ina ushawishi mkubwa na moto huo uliibua ghasia ambapo majeshi ya usalama yalifyatua risasi na kuua watu watatu.
Polisi wamesema wanachunguza afya yake ya kiakili.
Buganda ni falme kubwa kati ya nne zilizopo Uganda, zote ambazo hazina nguvu ya kisiasa.
Mabishano juu ya eneo baina ya Mfalme wa Baganda Ronald Mutebi na
Rais Yoweri Museveni kulisababisha ghasia mwaka 2009.

No comments: