


Baada ya kulemewa kwa maarifa na Barcelona mnamo cha kwanza, Arsenal walipambana kufa na kupona kutoka sare 2-2 katika uwanja wao wa Emirates.
Arsenal wangali na kibarua kigumu watakaposafiri hadi Uhispania kwa mechi ya marudio mnamo wiki mbili zijazo.
Katika mechi nyingine ya robo fainali Inter Milan iliitandika CSKA Moscow 1-0.
Barcelona walifanya mashambulizi makali mnamo kipindi cha kwanza huku Arsenal wakibaki kumshukuru kipa Manuel Almunia kwa kuwaokoa.
Hata hivyo uhodari wa Almunia ulitiwa dosari pindi tu kipindi cha pili kilipoanza.
Alifanya kosa la kuondoka kwenye goli na kumwachia mshambulizi Zlatan Ibrahimovic kumimina bao la kwanza.
Ibrahimovic aliongeza la pili huku matumaini ya Arsenal kudhibiti mchezo yakididimia.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alimwondoa Bacary Sagna na kumwachilia Theo Walcott kuwatatiza walinzi wa Barca.
Baada ya muda mfupi Walcott aliipatia Arsenal bao la kwanza.
Nahodha Cesc Fabregas aliongeza bao la pili kupitia penalti baada ya kuchezewa vibaya na Carles Puyol ambaye alitimuliwa kwa kadi nyekundu.
No comments:
Post a Comment