Kundi moja la walowezi wa Kizungu ambao walipokonywa ardhi yao na serikali ya Zimbabwe, limewasilisha kesi mahakamani, kutaka kumiliki mali ya serikali ya Zimbabwe ilioko Afrika Kusini.
Wakulima hao wanataka kumiliki ardhi na majengo ya serikali ya Zimbabwe, mjini Cape Town inayokisiwa kugharimu mamilioni ya dola, kama fidia ya kupoteza mashamba yao nchini Zimbabwe.
Uamuzi wao wa kwenda mahakamani, unafuatia ule uliotolewa na mahakama kuu nchini Afrika Kusini, kuwa hatua ya rais Robert Mugabe ya kuwapokonya walowezi hao mashamba ilikiuka sheria.
Uamuzi kama huo pia ulitolewa na kamati ya upatanishi ya nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
No comments:
Post a Comment