ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 30, 2010

Wazimbabwe 'washinda' Afrika Kusini

Mkulima atathmini uharibifu wa nyumba yake, Harare
Serikali ya Afrika Kusini imekabidhi umiliki wa nyaraka za nyumba moja ya Cape Town inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe kwa baadhi ya wakulima wa Zimbabwe.
Wakulima wa kizungu wanadai fidia kutokana na kunyang'anywa ardhi yao.
Serikali imepewa miezi miwili tu itoe fedha kwa ajili ya gharama za kisheria ilizolipa katika madai yao ya kutaka fidia la sivyo nyumba itauzwa.
Wiki iliyopita, mahakama ya Afrika Kusini ilikubaliana na uamuzi wa mahakama ya jimbo kwamba unyang'anyi wa ardhi kwa nguvu ni kinyume cha sheria.
Uamuzi huo umewapa fursa wakulima waliopoteza ardhi zao kuomba fidia katika mahakama za Afrika Kusini.

No comments: