Mwanasiasa mmoja wa upinzani nchini Burundi, amesema amekwepa mtego wa polisi wa kumkamata na kwa sasa yuko mafichoni, akihofia maisha yake.
Pancrase Cimapye, ambaye ni msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha FRODEBU, ameiambia BBC kuwa anaamini kuwa serikali inajaribu kumuangamiza.
Bwana Cimapye amesema kibali cha kukamatwa kwake kilitolewa baada ya kudai kwamba afisa mmoja wa cheo cha juu serikalini, alihusika na mauaji ya aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya kupambana na ufisadi nchini humo, Ernest Manirumva.
No comments:
Post a Comment