ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 6, 2010


Cuckovic-Nimerudi kivingine

Huku ikitarajia kuingia kambini kwa dhumuni la kujiandaa na mechi yao ya watani wao wa jadi 'Simba', itakayofanyika siku ya Jumapili hapa hapa jijini.



Kwani kipa wao Mserbia, Obren Cuckovic alitarajiwa kurejea nchini siku za usoni.

Naye Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kostadin Papic, ambaye pia alikuwa kwao Serbia kwa mapumziko, alisema amerudi na 'mbinu' mbalimbali za kuimaliza Simba na anawaahidi wanachama wa Yanga wasiwe na hofu yoyote juu ya mechi hiyo.

Kocha huyo alisema wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wanafanya mazoezi chini ya Kenny Mkapa, watakuwa na mazoezi makali chini yake.

Alisema hiyo hutokana na kutaka kumpa nafasi msaidizi wake mpya, Momo Medic, kuona uwezo wa wachezaji na kuanza kujipanga jinsi ya kuwapa mafunzo zaidi.

Kwani wamekuja na mambo mengi na kikosi hicho kitaanza mazoezi, huku wakiwa wamekamilika kwani Obren tayari yuko uwanja wa ndege (jana mchana) kwa ajili ya kurejea nchini.

Alisema kwamba likizo yake huko haikuwa nyepesi kwa sababu muda mwingi alikuwa akiutumia kuandaa programu mbalimbali, zikiwemo zile za mazoezi za timu yake pamoja na kufanya mazungumzo na wachezaji atakayowasajili katika msimu ujao wa ligi.

Alimalizia kwa kusema kwamba hajui kama mshambuliaji wake, Jerry Tegete, atarejea lini nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba akisema viongozi wa Yanga ndio wenye taarifa kamili za mchezaji huyo.



No comments: