ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 6, 2010

Stars kuumana na Zambia,Cambidge,Massachusetts

Stars
Zambia
Timu ya Stars inatarajiwa kupambana na Zambia hapo April 24 mwaka huu,mjini Cambridge,Massachusetts mpambano uliopaniwa na Wazambia.

Wazambia waishio Marekani hua na siku maalumu ya kuwa mwangalifu na ukimwi kila mwaka shughuli hizi hufanyika state tofauti,mwaka huu wanafanyia Massachusetts na hua na shughuli za michezo kama vile mpira wa miguu ambapo mwaka huu wameialika Timu ya Tanzania(Stars) kucheza na timu yao inayoundwa na golikipa aliyewahi kuichezea club ya Zamsure na timu ya taifa,wengine ni mabeki Aaron Simutowe aliyewahi kuchezea club ya Zanaco na timu ya taifa ya Zambia,atakuwa akisaidiwa na Peter Chitila na Emmanueli Chibale viungo wa timu hiyo ya Zambia ni Elton Kufa na Yonnah Banda mdogo wa mchezaji Cosmas Banda.

Washambuliaji wataongozwa na School boy international Patrick Daka(Sacred Heart University) na Mambo Phiri(Worcester State University).
Stars itakua chini ya magolikipa mahili Feisal Omar(mwana njenje)na Hakim Majaliwa(Mlandege),akisaidiwa na mabeki akili nyingi nguvu kidogo,Abdul-Latif Maalim,Muly Chomba,Lemy Mhando,Adam Jongo,Michael Mngodo,Adam Tenga,Libe Mwang'ombe(Germany Defense),Rashid(Beach Boy),Sultan na Evans Shangalai
Viungo ni Yahaya Kheri,Hadji,Helper,Elvis Dotto,Edgar Kisoka,Rahim Chomba,Francis Makala(Simba),Ally Hiral(Mpemba) na Juma Hadikubwa
Safu ya ushambuliaji itaongozwa na Gilles,Mudrick Majaliwa,Shabani Mwampambe,Hamfrey Owen,Inno Geofrey,Ebra Nyagaly,Denis Geofrey anechezea(Greensboro College,Nc),Vicent Ndusilo na Dullah Riyami

Mechi itachezewa stadium iliyopo,77Massachesetts Av,Cambridge,Ma.02139,Stars itachukulia mechi hii kama sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambano April 26 mwaka huu utakua umetimiza miaka 46,kwasababu hiyo basi tuna mipango ya kuuandikia ubalozi ituletee afisa balozi,Cambridge,Ma siku hiyo ya Mpambano.Tunaomba Wabongo Massachusetts wafike kwa wingi kuipa nguvu stars.

No comments: