ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 1, 2010

Haiti kupokea $10b ya shughuli za ukarabati


United Nations Secretary-General Ban Ki-moon discusses the climate deal reached in Copenhagen at a press briefing at U.N. headquarters December 21, 2009 in New York City. Ban said he welcomed the deal as an essential start to the process of battling climate change in spite of resistance from developing nations.  
 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameafiki ahadi za misaada zilizotolewa kwa taifa la Haiti ya dola billioni Kumi.
Ban amewaambia wajumbe wanaohudhuria kongamano la kimataifa kuhusu ukarabati wa Haiti kuwa kiwango hicho kimepita matarajio yao na ni kiwango ambacho taifa hilo linahitaji kwa ajili ya mwanzo mpya kufuatia tetemeko kubwa la ardhi Januari mwaka huu..
Nusu ya kiwango hicho kitatolewa katika kipindi cha miaka miwili ijayo na kilichosalia kitatolewa kwa ajili ya maendeleo ya kipindi kirefu.
Zaidi ya nchi 130 na mashirika kadhaa ya kimataifa yalihudhuria mkutano huo, huku nchi ya Marekani na Muungano wa Ulaya zikitoa kiwango kikubwa zaidi cha msaada huo.
Zaidi ya watu elfu mia mbili walifariki kufuatia tetemeko hilo la ardhi nchini Haiti na wengine zaidi ya milioni moja kuachwa bila makao.

No comments: