ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 2, 2010

Jeshi la Israel lashambulia Gaza.


[Country map of Gaza Strip]  
Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo kadhaa katika ukanda wa Gaza.
Msururu wa mashambulio hayo ya anga yalilenga majengo kadhaa, shamba na karakarana inayomilikiwa na kundi la Hamas, ambalo linathibiti eneo hilo la Gaza.
Ndege hizo za kijeshi zilirusha makombora manne karibu na mji wa Khan Younis ambako wanajeshi wawili wa Israel waliuawa wakati wa makabiliano kati yao na wapiganaji wa Kipalestina wiki iliopita.
Raia mmoja wa Gaza aliambia BBC kuwa wanajeshi wa Israel walisambaza makaratasi kuwaonya kuwa watalipisha kisasi kufuatia kuuawa kwa wenzao kabla ya mashambilizi hayo.
Mwandishi wa BBC katika eneo la Gaza anasema mashambulio hayo ya Israel ndio makubwa zaidi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

No comments: