Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Jenerali Scott Gration, ameanza mazungumzo ya dharura mjini Khartoum ya kujaribu kutatua mzozo kuhusu uchaguzi nchini humo.
Msemaji wa serikali ya Marekani amesema anaamini uchaguzi mkuu nchini Sudan unaweza kuokolewa hata baada ya vyama vingi vya upinzani kutangaza kuwa vimejiondoa.
Takriban vyama vyote vya upinzani nchini Sudan vimejiunga na chama cha kusini mwa nchi hiyo SPLM kususia uchaguzi wa Rais wa mwezi huu kwa kuhofia udanganyifu na hali ya usalama.
Kiongozi mkongwe wa kiislamu Hassan al-Turabi amethibitisha kwamba wagombea kutoka chama chake cha Popular Congress watashiriki kwenye uchaguzi.
No comments:
Post a Comment