ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 6, 2010

JK AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA


RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya kama ifuatavyo:- 

1. Gishuli M. Mbegesi - Njombe amepangiwa
kwenda Kilindi

2. Leonidas T. Gama - Mbeya amepangiwa kwenda Ilala
3. Frank A. Uhaula - Tarime
ameoangiwa kwenda
Kiteto

4. Bi. Sarah Dumba - Kilindi
amepangiwa kwenda Njombe

5. John B. Henjewele
- Kiteto
amepangiwa kwenda Tarime

6. Rashid M. Ndaile - Chunya amepangiwa kwenda
Mkinga

7. Evans Balama - Ilala
amepangiwa kwenda
Mbeya

8.Florence A. Horombe -Bukombe
amepangiwa kwenda Nzega

9. Bi. Zainab Kwikwega -Kasulu
amepangiwa kwenda Makete

10. Bi. Hawa Ngh’umbi -Makete
amepangiwa kwenda Bukombe

11. Lt. Col. John Mzurikwao -Mpanda
amepangiwa kwenda Sumbawanga

12. Bi Betty Machangu -Nzega
amepangiwa kwenda Kasulu

13. Dk. Rajab Lutengwe -Ulanga
amepangiwa kwenda Mpanda

14. Francis Miti
-Tandahimba amepangiwa kwenda Ulanga

15. Deodatus Kinawiro
-Mkinga amepangiwa kwenda
Chunya

Taarifa ya uteuzi huo iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Aggrey Mwanri imesema pamoja
na mabadiliko hayo, Rais Kikwete pia amemteua Bibi Husna Mwilima
aliekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Tandahimba kuchukua nafasi ya Ndugu Francis Miti ambaye anahamia wilaya
ya Ulanga.


Aidha, Rais Kikwete ametengua uteuzi wa Bw. Thobias M. Sijabaje ambaye alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la ugawaji wa
vocha za pembejeo za kilimo katika wilaya ya Sumbawanga katika msimu wa
mwaka 2009/2010.


Mabadiliko haya yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha utendaji katika wilaya
hizo na yanaanza mara moja.



Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S. L. P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumanne, Aprili 06, 2010.

No comments: