ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 5, 2010

Maharamia waiteka Meli ya Korea Kusini


 
Meli kubwa ya mafuta ya Singapore inayotumika na Korea Kusini kusafirishia mafuta imetekwa nyara na maharamia wa kisomali katika bahari Hindi.
Meli hiyo yenye tani elfu miatatu ijulikanayo kama Samho Dream, ilitekwa ikiwa imebeba mafuta ghafi kuelekea Marekani kutoka nchini Iraq.
Mahabaria ishirini na wanne walikuwemo kwenye meli hiyo ilipotekwa mnamo siku ya jumapili.
Korea kusini tayari imepeleka manowari yake ya kijeshi takriban kilomita elfu moja miatano kusini mashariki mwa Ghuba ya Aden, ambako inaaminika meli hiyo imetekwa, kuizuia kuelekezwa katika bandari yoyote.
Maharamia waliolenga kuteka meli katika fuo za Somalia mwaka jana, walijitajirisha kwa kulipwa mamilioni ya dola kama kikombozi.

No comments: