ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 5, 2010

Kiongozi wa ANC alaumiwa kwa mauaji


Waziri wa polisi nchini Afrika kusini Nathi Muthetwa amesema kuwa jaribio lolote la kulipiza kisasi kwa mauji ya mwanasiasa wa mrengo wa kulia aliyeuawa nchini humo Eugene Terreblanche halitasaidia kusuluhisha kwa vyovyote hali ilivyo sasa nchini humo.
Wafuasi wa mwanasiasa huyo aliyeunga mkono ubaguzi wa rangi, wamemlaumu kiongozi wa shirika la vijana la chama tawala cha ANC, Julius Malema kwa mauaji ya mwanasiasa huyo.
Msemaji wa chama cha Bw. Terreblanche cha Afrikaner Resistance Movement{AWB} amesema Malema anahusika na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi.
Kumekuwa na utata kufuatia lugha anayotumia Malema inayolaumiwa kuchochea chuki za rangi.
Wiki jana mahakama kuu ilimuamrisha Bw Malema dhidi ya kutumia wimbo uliotumiwa wakati wa harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi wenye maneno ''uwa Kaburu uwa mkulima''. Polisi wamesema Bw.

No comments: