Huku ushindani wa makampuni ya simu za viganjani yakiwa yameshika kasi ya ajabu,Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Reginald Mengi 'Ole Mengi' amenunua rasmi kampuni la Tigo.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana, mara baada ya utiaji saini makubaliano ya uuzaji wa rasilimali za Tigo, zenye thamani ya Dola 10.7 bilioni za kimarekani...Ole Mengi alisema hayo ni mapinduzi makubwa kwa wafanyabiashara wazawa na kuwaahidi watanzania huduma bora..ambapo kwa kuanzia amekuja na huduma mpya ambayo wateja wote Tigo kuanzia leo watapiga simu kwa nusu dk (sumni) kwa sekunde.
“Kuanzia kesho 'leo' waambieni watanzania tunawaletea huduma nyingine nzuri zaidi na lengo ni kumwezesha mtanzania yeyote kupata mawasiliano kwa gharama nafuu kabisa kuwahi kutokea. Sasa mteja wa Tigo ataweza kuzungumza kwa nusu shilingi (sumni) kwa wa maongezi,” alisema.
2 comments:
Her ya sikukuu bro!
hapo sawa
Post a Comment