ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 1, 2010

Idadi ya wajawazito wenye ukimwi inatisha!

 Pregnant woman in Tanzania by NewsHour. 
Hii ni picha imewekwa kama kielelezo  cha mama mjamzito sio muathilika wa ukimwi 


Idadi ya maambukizi kwa wajawazito ktk Manispaa ya Morogoro imekuwa kubwa na ya kutisha.

Wajawazito 6,691 waliojitokeza kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika Manispaa hiyo, kati yao 2,380 wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo katika kipindi cha Julai 2009 hadi Machi 2010.

Mratibu wa ukimwi katika Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana, alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya maambukizi ya ukimwi katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya.

Alisema manispaa hiyo ina jumla ya wajawazito 8,225 lakini waliojitokeza kupima ni 6,691 pekee.

Alisema pamoja na maambukizi hayo, lakini wananchi hususan mama wajawazito wamekuwa wakihamasika katika kujitokeza kupima VVU kwa hali ya juu.

Aidha, alisema kamati yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ongezeko la ukimwi, kwani bado liko juu na kwamba kamati hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maambukizi hayo.

No comments: