ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 1, 2010

Upinzani Sudan wasusia uchaguzi

Mohamed Osman al-Mirghani, mkuu wa chama cha Sudan Democratic UnionTakriban vyama vyote vya upinzani nchini Sudan vimejiunga na chama cha kusini mwa nchi hiyo SPLM kususia uchaguzi wa Rais wa mwezi huu kwa kuhofia udanganyifu na hali ya usalama.
Mwandishi James Copnall amesema hatua hiyo ni mtikisiko mkubwa kwa uchaguzi wa tarehe 11-13 mwezi huu, uchaguzi wa kwanza wa taifa unaohusisha vyama vingi katika kipindi cha miaka 24.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya kuwepo na mazungumzo yaliyosimamiwa na mjumbe wa Marekani Scott Gration.
Rais Omar al-Bashir, anayeshtakiwa kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita Darfur, sasa anakabiliwa na mpinzani mkuu mmoja tu.
Kiongozi mkongwe wa kiislamu Hassan al-Turabi amethibitisha kwamba wagombea kutoka chama chake cha Popular Congress watashiriki kwenye uchaguzi.

No comments: