ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 1, 2010

Jaribio la mapinduzi lafanyika G-Bissau


  
Imeripotiwa kuwa kundi la maafisa wa jeshi wa Guinea-Bissau wamemzuia mkuu wa majeshi na waziri mkuu Carlos Gomes katika jaribio la kupindua nchi.
Inaaminiwa Rais Malam Bacai Sanha amekuwa na mazungumzo na maafisa hao, wanaosema hawana nia ya kumpindua.
Awali, maafisa hao walitishia kumwuua waziri mkuu iwapo wafuasi wake wangeendelea kuandamana kwa kutaka aachiliwe.
Hali halisi ya nchi hiyo bado ina utata, lakini kumekuwa na matukio kadhaa ya mapinduzi tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974.
Vyanzo vya jeshi vimesema, mkuu wa majeshi Jenerali Jose Zamora Induta na maafisa wengine 40 wameshikiliwa katika mji mkuu wa Bissau.
Vyanzo hivyo vimesema, Jenerali Antonio Indjai, amechaguliwa kujaribu kutatua tatizo lililopo.
 

No comments: