
papa Benedict akiongoza sala ya pasaka uwanja wa St.Peter mjini Rome

maelfu ya waumini waliofurika uwanja wa St.Peter Mjini Rome
Mtakatifu Papa Benedict aliongoza sala ya pasaka mbele ya maelfu ya waumini waliofurika uwanja wa St.Peter mjini Rome bila kugusia mgogoro ulioikumba Kanisa Katoliki ya makasisi wanaohusika na kulawiti baadhi ya wasaidizi wao.
Msaidizi wa Papa, Cardinali Sodano aliyemtangulia Papa alisema katika hotuba ambayo haikutarajiwa kwamba wafuasi wa kanisa lake wanamuunga mkono na hawajachagizwa na shutuma alizozitaja kama umbeya kuhusiana na mgogoro wa makasisi.
Papa mwenyewe hakugusia kashfa hizo ila alizungumzia kwa ujumla kuhusu haja ya kanisa sio tu kupata furaha na matumaini bali pia masikitiko na unyonge, baada ya kusherehekea kufufuka kwa Yesu Kristu.
No comments:
Post a Comment