Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba
Mh.Suleiman Saleh akikagua kikosi cha Yanga
Mh.Suleiman Saleh akikagua timu ya Simba
Dedi Luba akijaribu kufunga kwa kichwa
Golikipa wa Yanga Feisal Omar(mwan Njenje) akiokoa moja ya hatari
Kocha ya Yanga Yasini Randi akiangalia gemu inavyokwenda
washabiki kaibao walihudhuria pambano
Mashabiki wa Yanga
washabiki kila kona
Ombye na Tifa
Mgeni wa Heshima Suleiman Saleh(kati) akiongea na Luka Kinyang'anyiro(shoto) na Rashid Mkakile(Bamchawi)
baada ya mpira washabiki wa Simba na Yanga walikua kitu kimoja
Ile mechi ya Simba na Yanga leo imeishia kwa Simba kula kipigo cha mabao 5-2 zidi ya mahasimu wao vijana wa jangwani,ni Simba ndio iliyokua na nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kwenye mpambano huo lakini wenzao wa Yanga ilionekana kuwazidi maarifa hasa kwenye kipindi cha pili.
Mpaka mapunziko timu zote zilikua zimefungana 2-2 mgeni wa heshima kuzikagua timu ambako Yanga walitaka mgeni wa heshima afisa balozi Mh.Suleiman Saleh aanze kwao badala ya Simba kwa wasi wasi kwamba bahati inaweza kua si yao kwa mpambano huo,na hii ilitokana na ushauri wa kamati ya ufundi ya wana jangwani hao.
mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakilisakama lango la Yanga kama nyuki lakini ulinzi mkali wa mabeki wa Yanga uliokua
ukiongozwa na Muly na Tif ukishirikiana Jongo na Jack wakisaidiwa na viungo Yahaya,Marley,na Haji uliweza kuzuia mashambulizi ya Simba.
Kunako dakika ya 30 Ebra Nyagaly aliandikia Yanga bao la kuongoza pale alipomchagua Kipa Julius Katanga na kumpeleka nyavu ndogo.
kuona hivyo Simba walimtoa beki wao wa kutumainiwa Rashid Beach Boy na kumuingiza Salum aliyeonekana njia ya mkato pale alipomsindikiza Haji alipozidiwa mbio na kufunga bao la pili kwa kiki kali iliyo muacha kipa wa Simba akigala asijue la kufanya.baada ya bao hilo Simba walizinduka usingizini na kuanza kuliandama goli la Yanga kama Simba aliye jeruhiwa na kuandika bao la kwa kunako dakika ya 40 bao lililogomewa na wachezaji wa Yanga kwa mfungaji Mashaka alimkanyaga kipa kabla ya kufunga baada ya kipa Feisal Omar(mwana Njenje) kuutema mpira uliopigwa kama adhabu ndogo na mchezaji hatari wa Simba Rahim,lakini kwa mshngao wa wengi Refa Mohamed Said kutoka misri alilikubali bao hilo.
bao hilo la Simba ni kama liliongezea timu hiyo ya msimbazi uhai na kuendelea kuwashambulia Yanga kama nyuki na kunako dakika ya 43 Shabani Mwaita aliwafungia Simba bao la kusawazisha kwa shuti kali ndani ya 18 na kumuacha kipa wa Yanga akiusindikiza mpira wavuni kwa macho.mpaka mapuziko timu zote zilikua 2-2
kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulishambulia goli la Simba,mashambulizi yaliyozaa matunda dakika 56 kwa supa sab Mussa alipofunga goli kwa shuti nje ya 18,goli hilo lilionekana kuwakatisha tamaa Simba kitu kilichofanya Yanga waendelee kuliandama goli la Simba kama Nyuki na kunako dakika ya 76 ni Haji tena aliyepeleka Msiba Msimbazi kwa kufunga goli zuri kwa krosi ilipigwa toka wingi ya kulia na Yahaya Kheri.
kunako dakika ya 86 Yanga walimuingiza Bingo Jr badala ya Dedi Luba ambaye dakika ya 88 alipigilia msumari wa mwisho na kuandika bao la 5,bao lililozima matumaini na ndoto za mahasimu hao kwa mwaka huu kua ni wao,Rashid Mkakile(Bamchawi) alisikika akisema wao kama Simba hawatacheza mechi na Yanga kwenye wanja hilo la Kalmia walisikika viongozi na wapenzi wakisema kiwanja hiki nuksi bora turudi Meadowbrook pk.kitendo kingine kilichokuwa si cha kawaida ni mchezaji wa kutumainiwa wa Yanga Hussein Ebrahim kuichezea Simba na baade ilibidi wamtoe kwa washabiki wakidai "mtoto Yanga huyo toa nje hawezi kuifunga timu yake"mpaka dakika 90 YANGA 5,SIMBA 2
No comments:
Post a Comment