ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 5, 2010

Waasi Congo wauteka uwanja wa ndege


Ramani ya Congo
Watu wenye silaha wameuteka uwanja wa ndege katika Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo, walipoushambulia mji wa kaskazini wa Mbandaka.
Askari mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini Ghana ameuawa katika shambuli hilo.
Imearifiwa kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na waasi wa kundi dogo la Enyele wapatao 100.
Hata hivyo kamanada mmoja amekanusha ripoti ya Umoja wa mataifa kwamba maafisa wameurejesha udhibiti wa uwanja huo wa ndege.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Kinshasa, Madnodje Mounoubai, ameiambia BBC kwamba, milio ya risasi imesikika usiku kucha na haijabainika kilichosababisha mashambulio hayo.

No comments: