
Viongozi waandamizi wa kidini Nigeria wameiambia BBC wamekutana na Rais Umaru Yar'Adua anayeendelea kuugua, wakisema anazungumza kwa shida.
Alikwenda Saudi Arabia kwa matibabu mwezi Novemba, na licha ya kurudi nyumbani hivi karibuni, bado hajaonekana mbele ya umma.
Viongozi hao wamesema waliweza kupeana mikono na kuzungumzia kilichokuwa kinaendelea wakati wa mkutano wao baada ya swala.
Kutokuwepo kwake nchini kulizua wasiwasi mkubwa Nigeria, na kusababisha makamu wake, Goodluck Jonathan kuchukua madaraka yake.
Mwandishi wa BBC Caroline Duffield mjini Lagos amesema ni mara ya kwanza kwa mtu ambaye si mwanafamilia kuzungumza na Rais huyo katika kipindi cha miezi kadhaa.
No comments:
Post a Comment