ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 2, 2010

Mtanange wa Yanga na Simba,Yanga matumbo juu yamhofia mgeni rasmi

Ule mpambano wa Simba na Yanga utakaofanyika jumapili april 4,homa imekua juu kwa kambi zote zaidi kwa Yanga inamuhofia mgeni rasmi wa mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa DMV na vitongoji vyake.

Mh.Suleiman Saleh
Mgeni rasmi ni afisa balozi Mh.Suleiman Saleh,aliyewahi kuwa msaidizi wa Mh.Mohammed Dewji(mbunge wa Singida mjini CCM),ambaye kampuni yake ya Mohammed Enterprises ilikua wadhamini wakuu wa Simba spots club(wana Lunyasi).

Washabiki na viongozi wa Yanga wameingiwa na wasiwasi mkubwa wakikumbuka mechi ya April 26 mwaka jana wakati mgeni rasmi alikuwa afisa balozi Doc.Switebert Mkama kwa habari zisizokua rasmi inasemekana ni Shabiki wa Simba na mechi hiyo Yanga walikula kisago 3-2 dhidi ya mahasimu hao wa msimbazi.

Shabiki wa Yanga akitabiri ushindi 3-0 zidi ya mahasimu hao wa msimbazi
Kambi ya msimbazi bado ipo kimya isipokua kocha Kenyata(Patrick Phiri) amehakikisha ushindi mnono kwa wanamsimbazi hao.Wakati huo huo kampuni ya Zion Home Care & Vizion one,inc,imetoa ahadi ya $100 kwa kila mchezaji na itawachomea nyama baada ya mechi wachezaji kama Simba itaibuka na ushindi.

Kocha wa Yanga Yasin Randi amesema vijana wake wapo gado tayari kukirudia kipigo kitakatifu cha september mwaka jana,tunamalizia mazoezi mepesi vijana wangu wamenihakikishia ushidi na wapo kwenye hali nzuri kimchezo.

Watabiri wanaipa nafasi kubwa Simba kuibuka na ushindi kwenye mapambano huo,kwa sababu ya wachezaji wengi wa Stars wanaokuja Dc akiwemo Francis Makala ni Simba,Stars ina mechi ya kirafiki na Maryland United siku ya jumamosi

No comments: